Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii

Utangulizi wa Kozi

Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii ni mfululizo wa warsha tisa, zilizoundwa kuwezesha makundi ya watu wazima na vijana kujifunza, kuthamini, na kuendeleza uhuru wa dini au imani (FORB) kwa wote katika jamii zao.
Nyenzo za kozi zinapatikana bure kwa mtu yeyote au shirika lolote kupakua na kutumia kwa namna wanayoona inafaa.

Hapa utapata taarifa kuhusu:

  • Mbinu ya ufundishaji wa kozi
  • Malengo ya kozi
  • Ni nani walengwa wa kozi
  • Ni nani anaweza kuratibu kozi
  • Mada zinazoshughulikiwa na kozi

Bofya hapa kupata nyenzo zote za kozi!

Tafuta nyenzo za kozi

Kozi hii inapatikana kwa lugha nyingi – je, lugha yako ipo?

Uwepo wa lugha zote

Mbinu ya Ufundishaji wa Kozi

Mbinu ya ufundishaji wa kozi hii inategemea usimulizi wa hadithi, mawasiliano ya kutazama, na mazoezi shirikishi yanayotegemea uzoefu wa washiriki katika maisha yao, jambo linaloifanya iwe rahisi kutumika hata katika mazingira yenye uelewa mdogo wa kusoma na kuandika.

Nyenzo hizi ni rahisi kubadilishwa kulingana na muktadha wowote na zimejaribiwa kwa mafanikio na waratibu wa ndani waliofanya kazi na washiriki wa dini mbalimbali nchini Nigeria, Tanzania, Jordan, India, na Uswidi, kwa mfano.

Kitu bora zaidi kuhusu kozi hii ni jinsi ilivyoshirikisha na kuendana na masuala yanayowahusu watu, huku ikiwa rahisi kufanywa kwa furaha tele. Ulikuwa uzoefu mzuri sana!

Hidaya Dude

Kituo cha Kidini cha Zanzibar, Tanzania

Malengo ya kozi

  • Kutusaidia kutambua na kukubali utofauti wetu na katika jamii
  • Kutufanya tuelewe na kuzikubali haki zetu za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya uhuru wa dini au imani
  • Kutambua matatizo yanayohusiana na uhuru wa dini au imani katika jamii zetu
  • Na kupata njia za kushughulikia matatizo kwa pamoja

Kozi hii inawalenga akina nani?

Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii inalenga watu wa ngazi ya jamii – wale wanaohisi kwamba kuna matatizo yanayohusiana na uhuru wa dini au imani katika jamii zao na wanataka kutafuta njia za kufanya mabadiliko.

Kozi hii haihitaji ujuzi wa awali, uzoefu, au hata kukubaliana na haki za binadamu kutoka kwa washiriki. Kinachohitajika ni mtu kuwa muwazi, awe na shauku ya kusaidia kujenga jamii za amani na usawa, na utayari wa kushiriki katika mchakato shirikishi wa kujifunza na kutafakari.

Imetayarishwa kwa ajili ya vikundi vya watu 12-24 lakini inaweza kubadilishwa ili kufaa vikundi vidogo au vikubwa zaidi.

Nani anaweza kuendesha kozi hii?

Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii ni shirikishi – inajumuisha mazoezi ya vikundi, michezo, hadithi, mijadala, na maigizo pamoja na mawasilisho. Yeyote mwenye uzoefu wa kuendesha mafunzo shirikishi kwa watu wazima na vijana anaweza kuendesha kozi hii. Kinachohitajika zaidi kwa mwezeshaji ni uelewa wa muktadha – uwezo wa kutathmini iwapo mada fulani ni nyeti sana au hatari kwa mijadala, na kurekebisha mchakato ipasavyo, pamoja na uwezo wa kushughulikia mienendo ya kundi endapo masuala nyeti au mvutano utatokea.

Huhitaji kuwa mtaalamu wa haki za binadamu au uhuru wa dini au imani ili kuendesha kozi hii. Habari zote muhimu zinatolewa, ikiwa ni pamoja na maandishi na mawasilisho kuhusu mada zinazohusika. Jukumu la mwezeshaji si kuwa mtaalamu, bali ni kuwaongoza washiriki kupitia mchakato wa kujifunza kwa pamoja.

Nyenzo za kozi

Nyenzo za kozi zinajumuisha mwongozo wa mwezeshaji pamoja na nyenzo zinazofuatana na kila kipindi, kama vile slaidi za PowerPoint, kadi za michezo, mabango, na maandiko ya mawasilisho.

Pata nyenzo zote za kozi hapa.

Muhtasari wa Kozi

Tunapenda kusikia uzoefu wako wa kutumia nyenzo za kozi kuleta mabadiliko katika jamii yako.

Tuambie hadithi yako!

Fomu ya maoni