Nyimbo za Filimbi na Ngoma

Rasilimali zinazoweza kupakuliwa

’Nyimbo za Filimbi na Ngoma’ ni hadithi inayowasaidia watu kutafakari kama wanathamini haki zinazolindwa na uhuru wa dini au imani.

Hadithi hii inafaa sana kwa kuwasaidia watoto, vijana na watu wazima kuchunguza mitazamo yao kuhusu haki hiyo bila kuizungumza moja kwa moja — jambo linaloifanya iwe muhimu zaidi katika mazingira magumu.

Iwapo unafanya kazi na vijana na watu wazima, unaweza kutumia hadithi hii pamoja na zoezi la majadiliano ’Hapo Zamani za Kale’, ambalo ni sehemu ya Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii (mtaala wetu wa kuhamasisha na kuelimisha jamii katika ngazi ya chini).

Katika ukurasa huu unaweza kupakua hadithi, mabango yenye michoro, slaidi za PowerPoint zenye michoro na maandiko ya masimulizi katika sehemu ya maelezo ya mzungumzaji, pamoja na karatasi ya zoezi la majadiliano.

‘Nyimbo za Filimbi na Ngoma’ na zoezi la ‘Hapo zamani za kale’ lilichochea mijadala ya kina. Lilifungua milango mingi ya fikra kwa washiriki. Walianza kutafakari kuhusu jamii zao – kutoka kwa miundo ya kijinsia hadi iwapo ni sawa kuvunja taratibu zilizopo.”

Hammam Haddad

Mwezeshaji, Jordanie

Ongeza ufahamu kuhusu uhuru wa dini au imani katika jamii yako

Tambua Kozi ya Wanamabadiliko wa Jamii

Bofya hapa